Thursday, 8 October 2015

Tagged Under:

Lubuva: Wasimamizi wa uchaguzi fuateni sheria

By: Unknown On: 02:48
  • Share The Gag

  • Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jji Mstaafu, Damian Lubuva akizungumza na wanahabari juu ya mambo yahusuyo tume hiyo.

    MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva amewataka wa wasimamizi wa uchaguzi na makamanda wa Polisi wa mikoa nchini, kufuata sheria ya uchaguzi na kutenda haki na haki hiyo ionekane ikitendeka siku ya uchaguzi mkuu.
    Aliyasema hayo jana jiji Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa waratibu wa uchaguzi wa mikoa, wasimamizi wa uchaguzi na makamanda wa polisi wa mikoa yote nchini na kanda maalum wapatao 800. Alisema ni vyema kujifunza makosa yaliyotokea kwenye chaguzi zilizopita na kujifunza ili katika uchaguzi huu mambo hayo yasijirudie.
    “Mmepewa jukumu kubwa la kuhakikisha uchaguzi huu unafanikiwa, fuateni sheria za uchaguzi, mfahamu kuwa dhamana ya ulinzi na uchaguzi huru na wa haki,” alisema Jaji Lubuva.
    Alisema uchaguzi huu unapaswa kufanyika kwa amani na uhuru na kuhakikisha na kwamba hawaruhusu vitendo vya uvunjifu wa amani ; au vile vinavyoonesha hatari ya kuvunjika kwa amani.
    Aidha alivionya vyama vya siasa na mawakala wao kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na NEC, za kuwataka wananchi wakishapiga kura waondoke vituoni kwani jukumu la ulinzi wa kura ni la tume hiyo na mawakala wao.
    Kwa upande wake, Mkuu Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu katika mkutano huo aliwataka wananchi kufuata sheria na utii wake ili kuepusha usumbufu, unaoweza kutokea wanapokaidi.
    Mangu alisema jeshi la polisi haliruhusu watu kubaki vituoni baada ya kupiga kura kwa sababu ya kuepusha mkusanyiko mkubwa usio na sababu; na kwamba kazi ya ulinzi wa kura uko mikononi mwa NEC na mawakala wa vyama vya siasa

    Chanzo Gazeti la HabariLeo

    0 comments:

    Post a Comment