Mgombea wa urais
kupitia tiketi ya chama cha CHADEMA Edward Lowassa amesema kuwa
hatokubali matokeo ya uchaguzi wa urais yanayoendelea kutolewa na Tume
ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (NEC).
Kiongozi huyo amesema kuwa ana ushahidi wa kutosha kwamba kuna udanganyifu uliofanyika.Amesema kuwa kura za chama hicho zimepunguzwa katika vituo vingi vya kupigia kura.
Akihutubia wanahabari pamoja na viongozi wengine wa upinzani, amesema kwamba kura zilizohesabiwa katika maeneo tofauti haziambatani na matokeo yaliyotolewa.
Lowassa ameongezea kwamba maeneo yote ambayo walipata ushindi yamecheleweshwa. Aidha, amelalamikia kukamatwa kwa maajenti wa chama hicho akidai kuwa ni ishara za kutaka kuiba kura.
Created by BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment