Teknolojia mpya ya habari na mawasiliano inamchango mkubwa sana kwenye uchaguzi wa mwaka huu, bila shaka imeongeza chachu ya ushindani kutokana jinsi ambavyo habari zinasambaa kwa muda mfupi ukilinganisha na chaguzi zilizopita.
Hata
hivyo, teknolojia hii imeibua wasiwasi mwingine kuwa huenda ikawa
inatumika katika kufanya udanganyifu kwa kuchezea (manipulate) picha
zinazoonekana kuwa za mikutano ya baadhi ya wagombea.
Dr.
Emmanuel Nchimbi, mjumbe wa kamati ya kampeni ya CCM ameeleza kwa
nyakati tofauti kuwa picha zinazoonekana za mikutano ya mgombea urais wa
Chadema, Edward Lowassa hazina uhalisia bali zimehaririwa ili kuonekana
kuwa alikuwa na watu wengi kwenye mikutano yake.
Baadhi
ya makada wa CCM kupitia mitandao ya kijamii wamekuwa wakieleza kuwa
picha inayosambaa ikionesha mafuriko ya Lowassa hivi karibuni jijini
Arusha sio ya kweli bali ni umati wa watu katika nchi moja ya Afrika
Magharibi.
Huu
ni muendelezo wa tuhuma za CCM dhidi ya Chadema kuhusu picha hizo kwani
Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Jakaya Kikwete aliwaeleza wananchi
waliohudhuria katika uzinduzi wa kampeni zake katika uwanja wa Jangwani,
Dar es Salaam, kuwa wasitishwe na picha za Chadema kwa kuwa
zimehaririwa na sio kweli.
“Wamechukua picha nyingine za mikutano ya Dk. Slaa, wanaunganisha, waambieni waje waone picha halisi,” alisema.
Hata
hivyo, Chadema na Ukawa kwa ujumla walimjibu mwenyekiti huyo wa CCM
katika siku ya uzinduzi wa kampeni zao uliohudhuriwa na maelfu ya watu
kwa kumtaka aione picha halisi ili aamini kuwa hakuna uhariri katika
picha anazoziona.
Je, ni kweli picha za Chadema zinahaririwa? Swali hilo tunawaachia watazamani wa mikutano hiyo
Credit; Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment