NA AZIZA MASOUD, DAR ES SALAAM
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), linaendelea kupunguza makali ya
mgawo wa umeme, baada ya kutangaza kuongeza megawati 125 ili kuhakikisha
huduma hiyo inarudi katika hali ya kawaida.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba, alisema
ili kuhakikisha nchi inarudi katika hali ya kawaida, mitambo
hiyo itawashwa kwa awamu ndani ya wiki hii ambapo juzi wameanza
kuwasha mtambo wa megawati 35 kutoka mtambo wa Symbion.
“Jana (juzi) mchana tuliwasha mtambo wa megawati 35 unaomlikiwa na
Symbion, na kuongeza kiwango cha umeme katika gridi ya taifa
na kupunguza tatizo la kukatika baadhi ya maeneo,” alisema Mramba.
Alisema megawati 90 zilizobaki zitawashwa wiki hii, ambapo mtambo wa
Kinyerezi unatarajia kutoa megawati 70, wakati mtambo wa Symbion utatoa
megawati nyingine 20.
Mramba alisema kupatikana kwa umeme huo, kutaendelea kuboresha huduma
ya nishati hiyo, hasa mikoa ya Arusha, Mwanza, Kilimanjaro, Mbeya na
Dodoma.
Alisema mahitaji ya umeme wakati wa mchana nchi nzima kwa siku
moja, ni megawati 870 na usiku megawati 940, wakati umeme unaozalishwa
ni megawati 720.
“Hali ya umeme itaendelea kuwa bora baada ya kuwashwa mitambo yote ya
Kinyerezi kutokana na kuwapo hali mbaya katika mabwawa yetu,” alisema
Mramba.
Alisema umeme unaozalishwa kwa maji, umepungua kwa asilimia 81.3 na kusababisha uhaba wa nishati hiyo.
Mramba alisema kuwashwa mitambo ya gesi, kumesaidia kupunguza makali ya mgawo.
Alisema kukatika umeme mara kwa mara kunasababisha shirika kupata hasara ya Sh milioni 50 kwa siku,
Created by Gazeti la Mtanzania
Thursday, 8 October 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment