Tuesday, 13 October 2015

Tagged Under:

Msaada wa chakula wahitajika Ethiopia

By: Unknown On: 23:10
  • Share The Gag
  • Mamilioni ya raia wa Ethiopia waliathirika wakati wa ukame mwaka 2011
    Zaidi ya watu milioni 8 nchini Ethiopia wanahitaji msaada wa dharura wa chakula kutokana na hali kali ya kiangazi ambayo imekumba baadhi ya maeneo ya taifa hilo.
    Ripoti ya Umoja wa mataifa ya afisi ya mipango ya misaada ya kibinaadamu OCHA inasema kuwa idadi hiyo ni maradufu ya idadi ya watu waliohitaji msaada miezi miwili iliopita.
    Umoja wa mataifa umeonya kuwa tekwimu hizo zinaweza kupanda hadi kufikia milioni 15 ifikiapo mwaka 2016.
    Uchunguzi uliofanywa na serikali na mashirika ya kimataifa ya misaada unasema ukame huo unatokana na mvua kukosa kunyesha katika misimu miwili iliyopita na pia kuanza kwa mvua kubwa ya El Nino.
    Maeneo yaliyoathirika zaidi ni Kaskazini, kati na Mashariki mwa Ethiopia ambapo watu milioni 8.2 wanakabiliwa na uhaba wa chakula.
    Pia watoto laki 35,000 wanakabiliwa na viwango vikubwa vya utapiya mlo.
    Aidha maelfu ya mifugo wamefariki katika maeneo kame ya Afar na Somali.
    Serikali inasema imetenga dola milioni 190 kukabiliana na janga hilo lakini Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya dola milioni 590 zitahitajika kukabiliana na ukame kati ya sasa na mwaka ujao.
    Wakati huohuo, idara ya utabiri wa hali ya anga imeonya kuwa mvua kubwa katika baadhi ya maeneo nchini huenda ikaharibu mazao shambani na kufanya hali hiyo kuwa mbaya zaidi.
    Miaka thelathini iliyopita Ethiopia ilikumbwa na kiangazi kikubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo, lakini sasa ni miongoni mwa nchi zenye uchumi unaokuwa kwa kasi zaidi barani Afrika.

    Created by BBC Swahili

    0 comments:

    Post a Comment