Madiwani wanaounda Umoja Katiba ya wananci (UKAWA) wakivutana na polisi baada ya kutokea vurugu
katika uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, zilizosababisha
kuahirishwa kwa uchaguzi huo katika ukumbi wa Karimjee.
VURUGU na fujo zimerindima jana katika uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, baada ya kuahirishwa tena kwa uchaguzi huo.
Katika vurugu hizo, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Theresa Mmbando
alifanyiwa fujo na wafuasi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (UKAWA), lakini polisi waliokuwa na mabomu pamoja na risasi,
walidhibiti hali hiyo.
Mmbando alijikuta akikabiliana na vurugu baada ya wafuasi hao wa
Ukawa na viongozi wao, wakiwemo wabunge na madiwani wa Chama cha
Wananchi (CUF), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kujaribu
kumvamia baada ya kutangaza kuahirishwa kwa uchaguzi huo.
Katibu Tawala huyo alisema uchaguzi huo, unaahirishwa hadi zuio
lililoandikwa tangu Februari 5 dhidi ya uchaguzi huo, lililokuwa
limebandikwa mlangoni mwa ukumbi wa Karimjee, litakaposikilizwa.
Kutokana na hali hiyo, askari Polisi walifika na magari ya Polisi
(defender) kuangalia usalama, wakamtoa Mmbando kwa mlango mwingine ili
kudhibiti vurugu hizo.
Wanachama wa Ukawa, walihoji ni kwa nini Mmbando atangaze kuahirishwa
kwa uchaguzi huo bila kubainisha ni nani aliweka zuio hilo.
Pia walihoji kama zuio hilo lilitolewa muda mrefu, kwanini watangaze jana bila ya kuandika barua kwa vyama husika.
Waliotoa hoja hizo ni pamoja na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge
wa Kibamba, John Mnyika, Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara na wanachama
wengine wanaounda umoja huo.
“Hatukubaliani na suala hili. Tunamuomba Rais atumie kaulimbiu yake
ya ‘Hapa Kazi Tu’ katika masuala makubwa kama haya ya umeya na wala
asifumbie macho,” alisema Mdee.
Chanzo HabariLeo.
Saturday, 27 February 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment