MGOMBEA ubunge Jimbo la Bunda Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Esther Bulaya, amelala mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi mjini Musoma, akidaiwa kutaka kuvamia Kituo cha Polisi Wilaya ya Bunda.
Bulaya, alikamatwa juzi jioni mjini Bunda pamoja na wafuasi sita wa chama hicho, kisha kusafirishwa usiku hadi mjini Musoma.
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya Bulaya na wenzake kuachiliwa kwa
dhamana jana, wakili wa chama hicho, Peter Makole, alisema kukamatwa kwa
mwanasiasa huyo ni njama zinazoendelea kufanywa na wapinzani wao ili
kumdhoofisha.
Alisema Bulaya na wenzake, wamefunguliwa kesi ya kutaka kujaribu kuvamia kituo cha polisi, jambo ambalo halina ukweli.
Makole
alisema Bulaya, alifika kituo cha polisi mjini Bunda juzi saa 11 jioni
kwa lengo la kumuona Kaimu Katibu wa Chadema Mkoa wa Mara, Kaunya
Yohana, aliyekuwa akishikiliwa kituoni hapo ili kujua sababu za
kukamatwa wake.
Alisema Bulaya na wenzake, wanatarajiwa kufikishwa mahakamni leo.
Kwa
upande wake, Bulaya alisema hizo ni njama za kutaka kumdhoofisha katika
kampeni yake ya kuwania ubunge, ambazo haziwezi kumkatisha tamaa, na
kuwaomba wapigakura wa jimbo hilo kutotishwa na matukio ya aina hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Philip Kalangi, hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo.
Credit; Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment