Shirika la habari
la taifa la Uchina, linaarifu kuwa afisa wa zamani ambaye anashutumiwa
kwa ufisadi mamilioni ya dola, amerejeshwa nyumbani kutoka Malaysia,
alikotorokea miaka mitatu iliyopita.
Zhan Zai-sheng, afisa wa
benki, anashutumiwa kuiba zaidi ya dola milioni, mia moja kwa kuvutia
rasilmali kwa njia isiyokuwa halali.Wakuu wanasema, alirejeshwa Uchina juma lilopita.
Awali mwaka huu, Uchina ilitoa orodha ya watu mia-moja wanaowatafuta, ambao wamekimbilia nchi za nje, wengi wao wakiwa na fedha nyingi.
Bwana Zhan Zai-sheng, anafikiriwa kuwa ni mtu wa 13 kurejeshwa nyumbani, katika orodha hiyo ya watu mia-moja.
Created by BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment