Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema kugundulika kwa gesi ya Bagamoyo mkoani Pwani itasaidia kuimarisha uchumi na ujenzi wa viwanda nchini.
Hayo aliyasema jana wilayani Bagamoyo katika mikutano yake
ya kampeni iliyofanyika katika majimbo ya Chalinze na Bagamoyo, ambapo
alisema gesi hiyo itasaidia ujenzi wa viwanda katika serikali yake.
"Kwanza niwapongeze kwa kugundua gesi hapa Bagamoyo, tena
imegunduliwa katika eneo la ruvu. Na hii itakuwa na manufaa kwa uchumi
wa Taifa na kwa wananchi wa Pwani kwa ujumla.
"Gesi hii itasaidia sana ujenzi wa viwanda vya kisasa
katika serikali ya Magufuli ya awamu ya tano. Tutajenga viwanda na
tutatoa ajira za uhakika kwa vijana wa nchi hii pamoja na Tanzania
yote," alisema Dk. Magufuli
Mgombea
wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea ubunge
wa jimbo la Bagamoyo Dk. Shukuru Kawambwa (kushoto) na jimbo la Chalinze
Ndugu Ridhiwani Kikwete kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye
viwanja vya shule ya Msingi Majengo,Bagamoyo.
Mgombea
wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge
wa jimbo la Bagamoyo Dk. Shukuru Kawambwa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Majengo,Bagamoyo.
Mgombea
wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge
wa jimbo jimbo la Chalinze
Ndugu Ridhiwani Kikwete kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Majengo,Bagamoyo.
Mgombea
ubunge
wa jimbo jimbo la Chalinze
Ndugu Ridhiwani Kikwete akimnadi mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John
Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya
shule ya Msingi Majengo,Bagamoyo.
Credit; Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment