SERIKALI imetenga kiasi cha fedha cha Sh. bilioni tano ( 5.93) ikiwa ni madeni ya mishahara ya Watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa(TALGWU) na Sh. bilioni nne(4) kwa ajili ya kulipa madeni ya yasiyohusu mishahara, fedha ambazo zitalipwa Oktoba mwaka huu.
Kauli
hiyo ya Serikali imetolewa leo na Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu wakati akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu madai na madeni ya watumishi hao kwenye
ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dares Salaam.
Aidha
Serikali imefafanua kwamba madai ya watumishi hao yanayohusu mishahara
mpaka kufikia Oktoba Mosi,mwaka huu,ambao si walimu malimbikizo yake
yalikuwa takribani Sh. bilioni 6.147, na idadi ya watumishi wanaodai ni
5,695 katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2015/2016.
Hivyo
hadi kufikia Oktoba , mwaka huu Serikali ilikuwa imewalipa watumishi
1,551 wakiwemo wa Serikali za Mitaa jumla ya Sh. bilioni 1.6 na malipo
hayo hayajumuishi yale yaliyofanyika kwa walimu.
“Aidha
Watumishi wa Serikali za Mitaa wapatao 455 wenye madai ya Sh.
milioni 593.2 watalipwa mwezi Oktoba, mwaka huu. Madai yaliyosalia
yataendelea kulipwa kila mwezi kadri uhakiki unavyokamilika,” alisema
Kaimu Katibu Mkuu huyo.
Alisema
kwa upande wa madai yasiyohusu mishahara , ambayo yamekuwa yakilipwa
kupitia fungu la Matumizi Mengineyo, madai ya kiasi Sh. bilioni 18
yalikwishahakikiwa na yanasubiri kulipwa.
Mkwizu aliongeza kwamba madeni hayo ya watumishi hao ni yale yaliyolimbikizwa hadi mwaka 2012/2013.
“
Serikali imepanga kulipa deni hilo lote katika kipindi cha kuanzia
Oktoba 2013 hadi Januari,2016,kwa kuanzia Oktoba 2015 Serikali imetenga
kiasi cha Sh. bilioni 4 na kiasi cha sh. bilioni 14 kitakachosalia
kitalipwa kwa awamu ndani ya kipindi kilichopangwa,” alisisitiza.
Aidha
Kaimu Katibu Mkuu huyo alisema wakati wa kutekeleza malipo hayo,
waajiri wameaagizwa kuwaandikia barua watumishi ambao madai yao
yamekataliwa au kupunguzwa ili kuwafahamisha sababu za kutakataliwa
kwake na hivyo kuwawezesha kuwa na taarifa sahihi kuhusu madai yao na
kuondoa uwezekano wa kudai mara nyingine.
Akizungumzia
kuhusu suala la uhakiki wa madeni alisema kwa upande wa madai
yasiyohusu mishahara yalikuwa ni sh. bilioni 18,lakini baada ya
kuhakikiwa yakafikia Sh. bilioni 14.
Alizitaja
sababu mbalimbali za kukataliwa baadhi ya madeni hayo kuwa ni zipo
tofauti na zinatokana na kutofuata sheria, kanuni na taratibu.
CreditMpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment