Jeshi la Marekani
limetoa zaidi ya tani 45 za silaha kwa waasi wanaopambana na wanamgambo
wa Islamic State (IS) kaskazini mashariki mwa Syria.
Jeshi hilo liliangusha shehena ya vifaa katika jimbo la Hassakeh, Msemaji wa wizara ya ulinzi wa Marekani ameeleza.Shehena hizo zimeripotiwa kuhusisha silaha ndogo ndogo,kubwa na maguruneti.
Hatua hiyo imekuja siku kadhaa baada ya Marekani kuacha mpango wa gharama ya dola za marekani milioni mia tano wa kuwafundisha maelfu ya waasi kupambana na IS
Badala yake imeelezwa kuwa fedha hizo zitatumika kugharimia silaha ambazo zitakuwa zinahitajika kwa makamanda wa makundi ya waasi ambao wako katika maeneo ya mapambano.
Created by BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment