Wizara ya afya huko
Gaza inasema mwanamke mmoja Mpalestina aliyekuwa mjamzito, na mwanawe
wameuawa katika shambulio lililofanywa na majeshi ya Israel huko .
Maafisa
hao wanasema nyumba ya mama huyo iliporomoka baada ya ndege za kijeshi
za israeli kufyatua makombora katika majumba yanayoaminika kuwa handaki
za wapiganaji wa Hamas.Mama huyo na mwanawe walishindwa kujinasua nyumba yao ilipoporomoka kutokana na kishindo hicho cha makombora mazito na hivyo kupoteza maisha yao.
Nyumba yao inasemekana kuwa mkabala na chuo cha kijeshi cha wanamgambo wa Hamas.
Ndege za kijeshi za Israeli zimeanza upya mashambulio huko Gaza huku kukiwa na wasiwasi wa hali hiyo ya makabiliano huenda ikazidi baina ya waisraeli na wa- Palestina .
Israeli inadai kuwa inalenga vituo vya silaha vya Hamas baada ya roketi mbili kurushwa huko Israel siku 2 zilizopita.
Hofu imetanda kwa mlipuko mpya wa mapigano husan baada ya waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu, kutoa amri askari wote wa akiba warejee kazini ilikuimarisha usalama katika mji wa Jerusalem unaotokota kwa uhasama baina ya wapalestistina na wayahudi.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani , John Kerry, amezunguzma na waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu na vile vile rais wa Palestinian Mahmoud Abbas kujaribu kuidhibiti hali hiyo.
Created by BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment