CHIZIKA! Wakati hekeheka za maandalizi zikipamba juu ya ndoa ya karne
ya staa wa sinema za Kibongo, Wolper, mwanadada huyo anaonekana
kuingiwa na ‘uchizi’ juu ya suala hilo ambapo muda wote anawaza ni kwa
namna gani ataweza kuweka historia juu ya shughuli yake. Akizungumza na
Ijumaa Wikienda, hivi karibuni ndani ya Ukumbi wa Jozi
Village, jijini Dar, Wolper alisema: “akili haijakaa sawa kabisa,
nawaza juu ya ndoa yangu ambayo muda si mrefu itatimia, silali, sili na
sipumui vizuri, kila kitu kimesimama, ni kama imenitia uchizi, muda wa
kuishi na mwanaume kwenye ndoa takatifu umewadia,” alitiririka Wolper.
Chanzo: GPL
Wednesday, 14 October 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment