TUME ya taifa ya Uchaguzi sasa imethibitisha kuwa wanafunzi wa Vyuo vikuu hawatapiga kura katika uchaguzi mkuu ujao.
Akizungumza
katika kipindi cha kikaangoni kinachorushwa na EATV, jana Emmanuel
Kawishe amesema kuwa wanafunzi hao hawataweza kupiga kura kuchagua
diwani,mbunge au Rais kwa kuwa sheria inasema kila mtu atapiga kura pale
alipojiandikishia.
“Sheria ya uchaguzi kifungu cha 61(3)a kuwa kila aliyejiandikisha atapiga kura alipojiandikisha” alisema Kawishe.
Aidha
amefafanua kuwa vituo vyote vya kupigia kura vitafunguliwa saa 1
asubuhi na vitafungwa saa kumi jioni hivyo kuwatahadharisha wapiga kura
wote kuwepo kituoni kabla muda wa kufunga.
Taarifa
ya kutopiga kura kwa wanafunzi wa vyuo vikuu imekuwa rasmi huku
viongozi wa Wanafunzi vyuo vikuu wakihangaika kupeleka shauri mahakamani
ili serikali ifungue vyuo kwa wakati na kuwapa wao fursa ya kupiga
kura.
Hii
ni mara ya pili kwa Vyuo vikuu kufunguliwa baada ya Oktoba, kwa mara ya
kwanza ilifanyika vile vile mwaka 2010 kwa kisingizio cha mikopo ya
Elimu ya juu.
Ushahidi
kutoka kwa wanafunzi mbalimbali waliowahi kunufaika na mikopo wanasema
serikali haijawahi kutoa mikopo kwa wakati licha ya sababu za mara kwa
mara kuahirisha kufungua vyuo wakati wa Uchaguzi.
Mapema
mwaka huu, Shirikisho la wanafunzi wa wanachadema wa Vyuo vikuu (Chaso)
kupitia Kaimu Mratibu wao Wilfred Mwalusanya aliitaka NEC kueleza
utaratibu wa kuwaandisha wanavyuo ili wakati wa kupiga kura waweze
kushiriki.
Tayari
tuhuma zimeanza kutolewa na wadau mbalimbali kuwa tume imetumiwa na
serikali ya CCM ili kuinusuru sababu wanavyuo wamehamasika kuelekea
uchaguzi mkuu mwaka huu.
Credit; Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment