Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mnyika alisema zipo mbinu
chafu na njama zinazofanywa na CCM ili kukihujumu chama hicho na
washirika wake na kwamba wamejipamba kukabiliana nazo.
Alidai
kwamba Chadema imegundua kuwapo kwa uandikishaji wa watu kwa BVR maeneo
mbalimbali nchini na kuwa njia pekee ya kudhibiti hilo ni tume
kukabidhi nakala ya orodha ya daftari la wananchi waliojiandikisha kwa
vyama vya siasa.
Hata
hivyo, wiki iliyopita NEC ilitangaza mpango wake wa kuwaalika wataalamu
wa mfumo wa Tehama wa vyama vya siasa pamoja na wale wa jumuiya za
kimataifa ili kuukagua mfumo wake wa kupokea na kuhesabu kura.
Kaimu
Mkuu wa Idara ya Elimu ya Mpigakura wa NEC, Giveness Aswile alisema
kazi hiyo itafanyika wakati wa kikao baina ya Tume na vyama vya siasa
mwishoni mwa wiki hii.
Pia
ilisema ipo katika hatua za mwisho kuhakiki taarifa katika daftari hilo
kabla ya kulibandika vituoni na kulisambaza kwa wadau.
Licha
ya kauli hiyo, Mnyika alisema: “Yanayoendelea kuhusu BVR yanadhihirisha
kuwa ipo haja kwa tume kukabidhi vyama vya siasa nakala ya daftari la
uandikishaji nchi nzima. Hii itatupa fursa sisi kuoanisha idadi ya
waliopo kwenye daftari. “
Ataka wasimsikilize Slaa
Katika
hatua nyingine, Mnyika amewataka wafuasi na wapenzi wa chama hicho
kupuuza kauli zinazotolewa na aliyekuwa Katibu Mkuu wake, Dk Willibrod
Slaa kwa madai kuwa kiongozi huyo hivi sasa amekuwa wakala wa chama
tawala.
Aliwataka
wapenzi wa Chadema wamuombee akisema amelamba matapishi yake ya
kuitetea CCM chama alichotumia muda wake kukipinga na kukikosoa.
Credit; Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment