Deo Filikunjombe akiweka sahihi katika fomu ya majina ya wabunge wasiokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda |
Bunge la Jamhuri ya Muungano halitamsahau marehemu Deo Filikunjombe, kwa umahiri na ujasiri wa kujenga hoja bungeni na kuikosoa serikali ya chama chake Chama cha Mapinduzi (CCM).
Alikuwa
hana hofu licha ya nyakati nyingine kuitwa mpinzani. Japokuwa alikuwa
mwanachama mwaminifu wa CCM, alijitihidi kujenga hoja ziliozokuwa na
mwonekano wa kitaifa zaidi, pasipo kuegemea siasa za chama chake. Baadhi
ya mambo atakayokumbukwa nayo ni pamoja na:
Shinikizo Kwa Waziri Mkuu
Ameacha
historia kwa uamuzi wake wa kutia saini fomu iliyoandaliwa bungeni na
kambi ya upinzani kukusanya saini za wabunge ili kwa pamoja kushinikiza
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ajiuzulu kutokana na Bunge kutokuwa na imani
naye.
Wabunge
hasa wa kambi ya upinzani walitaka Pinda ajiuzulu, kutokana na utendaji
usioridhisha na kuwataka wabunge bila kujali vyama vyao kumpa kiongozi
huyu wa shughuli za serikali bungeni, shinikizo la kuondoka.
Pinda
alitakiwa kujiuzulu kutokana na ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG), pamoja na taarifa za mwaka za Kamati za Kudumu
za Bunge za Hesabu za Serikali, Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma,
za kila mwaka kujaa ufisadi na ulaji wa fedha za umma, bila watuhumiwa
kuchukuliwa hatua.
Escrow
Filikunjombe alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesbu za Serikali (Pac).
Katika
kikao cha Bunge cha Novemba mwaka jana, akiwa na Mwenyekiti wa PAC,
Zitto Kabwe, waliwasilisha Ripoti ya PAC iliyochunguza uchotwaji wa
fedha katika akaunti ya Escrow, zilizokuwa zimehifadhiwa Benki Kuu
(BoT).
Hivi ndivyo alivyoshauri wakati akisoma ripoti ya PAC,:...”uteuzi
wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali utenguliwe mara moja na ashitakiwe kwa
matumizi mabaya ya ofisi yaliyosababisha upoteza mabilioni ya fedha za
umma…”
Kadhalika kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alimkosoa hivi: “Waziri
Mkuu alikuwa na taarifa zote kuhusiana kuchota fedha kwenye akaunti ya
Escrow, kwa mujibu wa ushahidi ulioletwa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa
Hesabu za Serikali (CAG), lakini hakuchukua hatua kuzuia muamala huo.
"Waziri
Mkuu alikuwa analijua jambo hili ndiyo maana katika maelezo yake
bungeni alilithibitishia Bunge kuwa fedha za Escrow hazikuwa za umma…”
Februari
2012, Filikunjombe alionyesha makeke zaidi pale alipomtaka aliyekuwa
Waziri wa Fedha, Mustapha Mkulo, pamoja na wa Kilimo, Chakula na
Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe, kujiuzulu nyadhifa zao kwa kushindwa
kutimiza ahadi ya Rais ya kununua mahindi kwa wakulima wa mikoani
wakiwa wa jimbo lake.
Shinikizo
hilo ni moja ya mambo yaliyomuondoa Waziri Mkulo kwenye wadhifa huo na
nafasi yake kuchukuliwa na Dk William Mgimwa, ambaye alifariki Januari
mwaka jana.
Mawaziri wavivu
Filikunjombe
alikosoa bungeni kuwa Tanzania haiendelei kwa kuwa mawaziri hawafanyi
kazi. Akichangia hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, alisema
wanaofanya kazi kikamilifu hawazidi 10.
Aidha wakati wa michango yake, aliliomba Bunge kubadilisha kanuni ili mawaziri wasiojibu maswali kikamilifu wapigwe viboko bungeni ili wakawaonyeshe wakwe zao.
Aidha wakati wa michango yake, aliliomba Bunge kubadilisha kanuni ili mawaziri wasiojibu maswali kikamilifu wapigwe viboko bungeni ili wakawaonyeshe wakwe zao.
Alikerwa na mawaziri kushindwa kujibu maswali kikamilifu na badala yake kufanya mizaha na kejeli kwa wabunge wanaouliza maswali.
Kutokana
na msimamo wake wa kuwavalia ‘njuga’ mawaziri wavivu, ambao mahala
pengine waliitwa ‘mawaziri mzigo’ alijijengea heshima kubwa machoni mwa
Watanzania wa kada zote na wenye itikadi tofauti za kisiasa.
Wakati
Fulani alidiriki kuwaambia wabunge wenzake wa CCM kuwa wasifikiri
wenzao wa upinzani ni maadui zao, bali maadui wanaoangusha chama chao,
ni watendaji serikalini, ambao hawatimizi majukumu yao ya kuwatumikia
wananchi.
Kutounga mkono hoja
Hakuogopa
kusema ukweli, kwenye vikao vya Bunge mwaka huu, alikataa kuunga mkono
hoja ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa Bunge la Bajeti. Hakuwa mtu wa
kuburuzwa.
Kutokana
na msimamo wake, wakati mwingine alikuwa akizungumza `lugha moja’ na
wabunge wa upinzani, kuliko wale wa chama chake, CCM.
Aliikosoa
serikali kuwa siyo sikivu na imekuwa na uzembe katika utekelezaji wa
mambo muhimu na haichukui hatua kwa viongozi na watendaji wabadhirifu,
mafisadi na wasiotimiza wajibu wa kutumikia umma.
Katika kushughulikia ufisadi, Filikunjombe hakuwa na simile na wakati wote akiwa mbunge alipiga vita uhalifu huo.
Katika kushughulikia ufisadi, Filikunjombe hakuwa na simile na wakati wote akiwa mbunge alipiga vita uhalifu huo.
Credit, Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment