Nyerere alisema hayo katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Sokoine, Serengeti mkoani Mara.
“Lowassa
wamekutukana sana na wengine wanasema wewe mgonjwa, sasa sisi tumesema
Mkoa wa Mara tunamchagua mgonjwa ili ashughulikie masuala ya hospitali
zetu kwa kuwa hilo ndilo tatizo kubwa.
“Rais
ambaye akiweka sahihi mtu ananyongwa, sahihi yake inaruhusu nchi
kuingia vitani, anazungumza kuwa atajenga Mahakama za kufunga wezi na
mafisadi, wakati ukienda magereza waliojaa ni walala hoi… sisi watu wa
Mkoa wa Mara tunasema hatuhitaji mahakama za mafisadi, tunahitaji
hospitali bora,” alisema Nyerere.
Huku
akishangiliwa na umati wa waliofika kumsikiliza, Nyerere alisema pia
kuwa baba yake mkubwa, hayati Mwalimu Julius Nyerere alitawala kwa miaka
23 lakini hakuwahi kutoa kauli za kibabe.
Akihutubia
mkutano huo wa kampeni, Lowassa aliahidi kujenga barabara ya lami
kuanzia Makutano hadi Mto wa Mbu kupitia Mugumu iwapo atachaguliwa na
kusema anakusudia kumaliza matatizo yanayoisumbua wilaya hiyo ikiwamo
barabara, chujio la maji, migogoro ya wanyama na wananchi na hospitali
ili kuhakikisha wananchi wa wilaya hiyo wanafaidi matunda ya nchi.
“Wingi
wenu ni ishara kubwa kuwa mnataka mabadiliko ya kweli, natambua mnayo
matatizo mengi hapa, ninaombeni mtumie wingi wenu huu kunipigia kura,
mbunge na madiwani ili tuweze kuleta mabadiliko, nasisitiza nipeni
mgombea ubunge ili tushirikiane kukamilisha matatizo hayo ikiwamo
barabara,” alisema.
Hivi
karibuni, akiwahutubia wakazi wa Mji wa Mugumu, mgombea mwenza wa CCM,
Samia Suluhu Hassan alisema wakichaguliwa, watahakikisha barabara hiyo
inajengwa kwa kiwango cha lami.
Lowassa
alisema anakerwa na mfumo ambao umeanza kujengeka wa wanyama
kuthaminiwa kuliko wananchi, pamoja na kurejea kauli yake kuwa serikali
yake itachunguza upya suala la Operesheni Tokomeza ili waliopata madhara
wafidiwe huku akisisitiza kurudisha heshima ya wananchi kuthaminiwa
badala ya wanyama.
Kuhusu bodaboda, aliahidi kuwa serikali atakayounda itawatafutia benki ili wakopeshwe.
“Katika
nchi zilizoendelea kundi kama hili la bodaboda, serikali inawajibika
kuwalipa kwa kuwa hawana ajira… hapa pamoja na kushindwa kuwatafutia
mitaji, wamebaki kuwafukuza na kuwapiga, lazima hayo yakomeshwe na
watakuwa marafiki zangu,” alisema.
Akimnadi
mgombea ubunge jimbo hilo, Marwa Ryoba na madiwani wa kata 30, Lowassa
aliwataka wananchi kutobweteka, bali wahakikishe wanajitokeza kwa wingi
kwenda kupiga kura na kwamba hiyo ndiyo itakuwa silaha pekee ya kuiondoa
CCM na kuiweka ya Ukawa ili iwaletee mabadiliko ambayo yameshindikana
kwa muda mrefu.
Waziri
Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye aliwataka wananchi wasimchague mgombea
wa urais wa CCM kwa kuwa hana sifa za kuwa kiongozi mkuu, haambiliki na
hapokei ushauri wa wengine.
“Nimekuwa
Waziri Mkuu kwa miaka 10, Lowassa na Magufuli walikuwa mawaziri chini
yangu, najua utendaji wao, Lowassa ni mtu wa kutafakari kwanza kabla ya
kuchukua hatua, lakini huyu Magufuli anahitaji kuwa chini ya mtu...
kauli zake za sasa hata ninyi mmesikia huyu alipaswa kuwa waziri chini
ya mtu,” alisema.
Sumaye
alisema wananchi wanatakiwa kumpima kwa kauli zake ambazo anatoa kwa
sasa ikiwa ni pamoja na kushughulikia mafisadi na wala rushwa ndani ya
Serikali ya sasa ambayo na yeye ni miongoni mwao.
“Wao
wanapita na kututukana lakini sisi tunaeleza ukweli mtupu, kama ufisadi
umemshinda ndani ya wizara yake anawezaje ngazi ya urais? Amelazimisha
kununua meli mbovu iliyotumika kwa zaidi ya miaka 30 ambayo walitarajia
iwe inafanya safari zake kwenda Bagamoyo, sasa wameipeleka Kusini,
nawaambia Watanzania mtajuta,” alisema.
Alisema
miongoni mwa matatizo yatakayoikuta serikali itakayoundwa na Lowassa
endapo atachaguliwa ni kulipa madeni makubwa ya nje ambayo yamefikia
zaidi ya Sh35trilioni.
Alisema wakati hali ya maisha inazidi kuwa ngumu kutokana na matumizi mabaya ya CCM ikiwamo safari zaidi ya 412 za Rais zilizotumia zaidi ya Sh4trilioni kwa kipindi cha miaka 10, Dk Magufuli amezisifia kuwa zimetusaidia na kuongeza kuwa hiyo inaashiria kuwa wakimchagua huenda akatembea zaidi ya mtangulizi wake.
Alisema wakati hali ya maisha inazidi kuwa ngumu kutokana na matumizi mabaya ya CCM ikiwamo safari zaidi ya 412 za Rais zilizotumia zaidi ya Sh4trilioni kwa kipindi cha miaka 10, Dk Magufuli amezisifia kuwa zimetusaidia na kuongeza kuwa hiyo inaashiria kuwa wakimchagua huenda akatembea zaidi ya mtangulizi wake.
Alibainisha
kuwa mfumo ndani ya CCM ni mbovu ndiyo maana watu wengi wanakimbia, kwa
kuwa fedha za umma zinachotwa na watu na kuanzisha kampuni kubwa ambazo
huandika majina ya watoto wadogo hata wa miaka mitatu, huku watoto
wengine wakikosa madawati na dawa hospitalini hakuna.
Kabla ya mkutano
Shughuli
nyingi mjini Mugumu zilisimama na watu walijaa uwanjani hapo kuanzia
saa mbili asubuhi, eneo hilo likipambwa kwa bendera na mabango ya
mgombea huyo. Aliwasili saa sita mchana na kuhutubia na baadaye kuelekea
Nyamongo wilayani Tarime.
Credit;Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment