Tuesday, 13 October 2015

Tagged Under:

Kikwete ataka NIMR itafiti magonjwa yasiyoambukiza

By: Unknown On: 23:24
  • Share The Gag

  • Rais Jakaya Kikwete.

    RAIS Jakaya Kikwete ameiagiza Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), kujikita zaidi kutafiti magonjwa yasiyoambukiza kwa sababu watu wengi wanaugua magonjwa hayo kwa sasa.
    Rais Kikwete alisema hayo katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue katika kongamano la sayansi la 29, lililoandaliwa na taasisi hiyo na kufanyika jana Dar es Salaam.
    Katika taarifa hiyo, Kikwete alisema kuwa kipindi cha miaka ya nyuma, magonjwa ya kuambukiza ndio yaliyokuwa yakisumbua zaidi, lakini sasa magonjwa yasiyo ambukiza kama vile saratani ndio yamezidi kushika kasi na kuathiri watu wengi Alitaja magonjwa mengine yasiyoambukiza na ambayo yanasumbua wengi kuwa ni kisukari, magonjwa ya moyo pamoja na yanayoathiri mfumo wa kupumua.
    Rais alisema, “Magonjwa hayo yamekuwa tishio zaidi nchini hivyo NIMR ijikite kuyafanyia utafiti pia”. Alisisitiza kuwa, serikali ipo tayari kusaidia utafiti wa kisayansi ili kuimarisha afya za watanzania.
    Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Dk Mwele Malecela alimpongeza Rais Kikwete kwa kuweka bajeti ya asilimia moja kwa ajili ya utafiti na kuiomba serikali kuongeza fungu katika eneo hilo, ili kukabiliana na changamoto mbalimbali kwenye utafiti.
    “Ingawa tunategemea fedha za ndani kwa ajili ya kufanta utafiti tunaotaka sisi, upatikanaji wa fedha hizo bado ni tatizo. Hata hivyo, tunajitahidi kuhakikisha tunaendesha utafiti wetu kwa umakini licha ya uhaba wa fedha,” Dk Malecela alisema.

    Created by Gazeti la HabariLeo.

    0 comments:

    Post a Comment