MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chadema kupitia mwamvuli wa Ukawa, Edward Lowassa, anatarajia kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrati (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, imefahamika.
Duru
za siasa kutoka ndani ya Ukawa, zimebainisha kwamba, licha ya
kusambazwa kwenye mitandao kwa taarifa za Mchungaji Mtikila kumshambulia
Lowassa kwa maneno kabla ya kifo chake, lakini mgombea huyo wa Ukawa
amepanga kwenda kuhudhuria mazishi hayo kutokana na sababu kadhaa.
“Kwanza
amesema Mtikila ni miongoni mwa waasisi wa siasa za mageuzi nchini na
ametoa mchango mkubwa katika mambo mbalimbali yaliyobadilisha demokrasia
na kupanua wigo wa siasa za upinzani,” kilisema chanzo kutoka ndani ya Ukawa.
Lakini
pili, kwa mujibu wa chanzo hicho, ni kushindwa kuhudhuria misiba kadhaa
ya wanasiasa waliofariki dunia katika kipindi hiki cha kuelekea
uchaguzi mkuu.
“Hakuhudhuria
msiba wa Peter Kisumo kutokana na kususa baada ya msafara wake
kuzuiliwa, lakini hakwenda kumzika mgombea wa Chadema katika Jimbo la
Lushoto, Mohammed Mtoi na hakuhudhuria msiba wa aliyekuwa Waziri wa
Utumishi, Celina Kombani, ambaye alikuwa anatetea kiti chake katika
Jimbo la Ulanga Mashariki kupitia CCM,” kilibainisha chanzo hicho.
Mchungaji
Mtikila alifariki kwa ajali ya gari Jumapili, Oktoba 4, 2015 katika
Kijiji cha Msolwa mkoani Pwani wakati akirejea Dar es Salaam kutoka
Njombe alikokwenda kufanya mkutano wa hadhara.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi ya mwanasiasa huyo, David Mwaijojele, mwili wa marehemu utasafirishwa leo kwenda Ludewa, Njombe na endapo kila kitu kitakwenda sawa, Mchungaji Mtikila atapumzishwa kaburini kesho.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi ya mwanasiasa huyo, David Mwaijojele, mwili wa marehemu utasafirishwa leo kwenda Ludewa, Njombe na endapo kila kitu kitakwenda sawa, Mchungaji Mtikila atapumzishwa kaburini kesho.
Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment