Wanajeshi wa
Cameroon wanasema kuwa kumetokea mashambulio mawili sambamba ya
kujitolea mhanga, kaskazini mwa nchi, karibu na mpaka wa Nigeria.
Milipuko hiyo karibu na Mora imeuwa watu kama 9, na kujeruhi zaidi ya 10.Baadhi ya ripoti zinaeleza kuwa washambuliaji wote wawili walikuwa wanawake.
Kundi la wapiganaji Waislamu, Boko Haram, limefanya mashambulio ya mara kwa mara katika eneo hilo.
Created by BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment