MJUMBE wa Kamati ya Kampeni wa CCM, Christopher ole Sendeka |
Alisema kwa hali hiyo huwezi kuwalinganisha Dk Magufuli na Lowassa, kwani jina la mgombea wa CCM liko juu na atapata kura nyingi halali za Watanzania na ndiye atakuwa Rais wa Tano wa Tanzania.
Sendeka alisema kwa sasa CCM inachoshindanisha ni mkoa upi utatoa kura nyingi kwa Dk Magufuli, na si itashindaje kwani tayari kuna uhakika wa kushinda kwa kishindo.
Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni katika uwanja wa Shule ya Msingi Ngedere katika eneo la Nyakato Jimbo la Ilemela mjini hapa, ambako alikuwa akimnadi mgombea mwenza wa CCM, Samia Suluhu Hassan, Sendeka alisema Dk Magufuli anakubalika Monduli ambako ni kwao Lowassa na Karatu ambako kulikuwa ngome ya Chadema.
“Kule Kilimanjaro wanasema ni Magufuli tu ndiye Rais wetu, hivyo na nyinyi hapa semeni bila kigugumizi ukiulizwa Rais wako ni nani sema ni Dk Magufuli,” alisema Sendeka.
Created by Gazeti la HabariLeo
0 comments:
Post a Comment