Timu ya Taifa ya
Tanzania itajitupa uwanja Novemba 14 kukipiga na timu ya taifa ya
Algeria ikiwa ni hatua ya pili kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la
Dunia zitakazofanyika mwaka 2018 nchini Urusi
Katika mchezo huo Stars wataanzia nyumbani katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam.Mchezo wa marudiano utakuwa huko nchini Algeria siku tatu baadae ambapo Mbweha hao wa Jangwani watakua ndio wenyeji wa mtanange huo.
Kikosi cha Stars chini ya Kocha Mkuu Charles Mkwasa kimefanikiwa kusonga hatua ya pili ya michuano hiyo baada ya kuiondosha Malawi (The Flames) kwa jumla ya mabao 2-1, nyumbani ikishinda 2-0, na kufungwa 1 – 0 jijini Blantyre.
created by BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment