Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mgombea
Urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, na Mgombea Mwenza, Ndugu Samia
Hassan Suluhu, wameendelea kufanya kampeni katika maeneo mbalimbali
nchini..
Hadi jana, tarehe 10.10.2015, Dkt. Magufuli alikuwa
amekwishatembelea Mikoa 22 na Majimbo 203.
Amekwishafanya mikutano mikubwa rasmi 240 na mikutano 865 ya kusimamishwa na wananchi njiani, hasa wananchi wa vijijini. Dkt. Magufuli amekuwa akitumia usafiri wa barabarani, ambapo hadi sasa ametembea kilomita 31,467 kwa barabara kuu, barabara za mikoa, barabara za wilaya, barabara za mlisho (feeder roads), na barabara za mijini na vijijini.
Amekwishafanya mikutano mikubwa rasmi 240 na mikutano 865 ya kusimamishwa na wananchi njiani, hasa wananchi wa vijijini. Dkt. Magufuli amekuwa akitumia usafiri wa barabarani, ambapo hadi sasa ametembea kilomita 31,467 kwa barabara kuu, barabara za mikoa, barabara za wilaya, barabara za mlisho (feeder roads), na barabara za mijini na vijijini.
Watu wengi wamekuwa
wanajitokeza kwenye mikutano yetu. Lakini la muhimu zaidi ni hamasa na
matumaini wanayopata baada ya kumuona jukwaani na kumsikiliza Dkt.
Magufuli.
Wananchi wanapoondoka kwenye mikutano yetu ya kampeni wanakuwa wamepata fursa ya kumsikia mgombea wetu kwa kitambo kinachotosheleza, wamemuelewa, wameelewa sera za CCM na wameshawishika kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi.
Wananchi wanapoondoka kwenye mikutano yetu ya kampeni wanakuwa wamepata fursa ya kumsikia mgombea wetu kwa kitambo kinachotosheleza, wamemuelewa, wameelewa sera za CCM na wameshawishika kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi.
Tunaingia katika ngwe ya mwisho ya kampeni
zetu. Tangu kampeni zianze hadi sasa, ushindi wa CCM unajidhihirisha.
Hata hivyo, katika kujihakikishia ushindi na kuongeza kiwango cha
ushindi, katika ngwe hii ya mwisho, tumeanza kampeni nzito.
Katibu
Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana, ameanza ziara ya kampeni katika
majimbo 64. Vilevile, viongozi wengine wa CCM, akiwemo Rais na
Mwenyekiti wa CCM Mstaafu Mzee Benjamin William Mkapa, nao wataanza
safari za kuzunguka nchi nzima kumuongezea kura Dkt. Magufuli na
wagombea wetu wa Ubunge na Udiwani.
Tutatumia helikopta nne kwa
ajili ya shughuli hii. Dkt. Magufuli na Ndugu Suluhu wataendelea kutumia
usafiri wa gari hadi mwisho wa kampeni, isipokuwa pale tu itakapokuwa
hakuna budi.
Maandalizi ya Kuleta Mabadiliko ya Haraka na ya Kweli
Pia,
tunapenda kutoa taarifa kwamba, mgombea wetu, Dkt. John Pombe Magufuli,
ameunda jopo la wanataaluma na wataalamu huru magwiji wazalendo wa
uchumi, biashara, utawala na sheria, kutoka kwenye taasisi za elimu ya
juu, asasi zisizo za kiraia, na sekta binafsi, kwa ajili ya maandalizi
ya kufanya mabadiliko makubwa Serikalini kuanzia siku ya kwanza
atakayokuwa madarakani.
Dkt. Magufuli amelipa jopo hili majukumu yafuatayo:
1.
Kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo Serikali itabana matumizi,
ikiwemo manunuzi ya umma, posho za vikao na matumizi ya magari, ili atoe
maamuzi kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa;
2. Kuchunguza na
kupendekeza maeneo ambayo Serikali itaongeza mapato mara moja bila hatua
za kibajeti kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa;
3. Kuchunguza na kupendekeza maboresho makubwa katika mfumo wa utendaji na utumishi na ufanisi katika Serikali;
4.
Kupitia kodi na ushuru wenye usumbufu kwa wafanyabiashara wa ngazi
zote, wakulima, wafugaji na wavuvi iwapo unaweza kurekebishwa bila
kuathiri bajeti ya Serikali inayotekelezwa sasa.
5. Kupitia
sheria zote za nchi na kuorodhesha Sheria ambazo zinapaswa kubadilishwa
haraka ili kuharakisha mabadiliko ya kweli na ya haraka ambayo
ameyaahidi kwa Watanzania;
6. Kupitia na kuorodhesha masuala yote
na kero zote zinazosubiri maamuzi ya Serikali ili atoe maamuzi kuanzia
siku ya kwanza atakapoapishwa.
7. Kupendekeza miundo na idadi ya
Wizara na kutengeneza rasimu za mikataba ya kazi kwa Mawaziri, Makatibu
Wakuu na watendaji wengine wakuu atakaowateua mara baada ya kuapishwa.
8.
Kupendekeza njia za haraka za kumaliza kero za watumishi wa umma, hasa
walimu, askari, madaktari na wauguzi, ili aanze nao kazi wakiwa na ari
na morali ya kusukuma mabadiliko ya kweli.
9. Kutengeneza rasimu
ya mpango-kazi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM na ahadi alizozitoa kwenye
kampeni, hasa upatikanaji wa ajira kwa haraka na umeme wa uhakika;
10.
Kupendekeza muundo wa kitaasisi na utaratibu muafaka wa kutekeleza
ahadi ya kutoa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji na mtaa nchini.
Dkt. Magufuli ameazimia kuanza kazi mara moja kwa bidii kubwa na maarifa mapya.
Imetolewa na:-
January Makamba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Mjumbe wa Kamati ya Kampen
credit; Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment