Msanii wa filamu, Dr Cheni amesema kuwa biashara ya filamu kwa sasa imeshuka kutokana na tatizo la umeme linaloendelea.
Dr Cheni ameambia Bongo5 kuwa mawakala wanalalamika kushindwa kuuza
kazi za filamu kama walivyotarajia kutokana na tatizo la umeme.
“Soko la filamu sasa hivi linasumbua kutokana na haya matatizo ya
umeme,” amesema Cheni. “Umeme ukisumbua na soko la filamu linayumba kwa
sababu sisi wateja wetu wanatumia umeme, sasa hata wazalishaji wa kazi
zetu wanaogopa kuzalisha kazi nyingi kutokana na kutonunulika sokoni.
Yaani kwa kifupi soko limesimama. Wewe nenda kwa mawakala pale Kariakoo
watakwambia. Kwahiyo ukiona tatizo la umeme ujue na sasa kazi zetu
zinasimama.”
Chanzo: GPL
Saturday, 10 October 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment