Matokeo ya ukaguzi
wa kimatibabu uliofanyiwa mabaki ya mwili wa aliyekuwa rais wa Burkina
Faso marehemu Thomas Sankara miaka 28 baada ya kuuawa, yanaonyesha kuwa
mwili wake ulijaa risasi kulingana na wakili aliyekuwa akiwakilisha
familia.
Haya ni kwa mujibu wa ukurasa wa Facebook wa kituo cha habari cha Burkina 24.Familia yake ilikuwa ikisubiri matokeo ya DNA kuthibitisha kwamba mabaki hayo yalikuwa ya Bw Sankara, wakili Benewende Sankara aliviambia vyombo vya habari nchini humo.
Bwana Sankara aliuawa katika mazingira ya kutatanisha akiwa na umri wa miaka 37 na kundi la wanajeshi mwezi Octoba mwaka 1987, na alizikwa kwa haraka kufuatia mpainduzi yalioongozwa na mrithi wake Blaise Compaore.
Created by BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment