Mgombea
huyo wa CCM aliyasema hayo katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana
mkoani Lindi na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wafuasi wa chama hicho,
ambapo alisema kuwa baadhi ya wagombea wa vyama vya upinzani ndio chanzo
cha tatizo la umeme nchini kwa kuwa ‘walipiga deal’ kupitia makampuni
ya ufuaji umeme.
Katika
hatua nyingine, Dkt. Magufuli, alisema amepata taarifa kwamba kuna
njama zinaandaliwa kwa lengo la kumuangusha mgombea ubunge Jimbo la
Mtama kwa tiketi ya chama hicho, Nape Nnauye.
Dk. Magufuli aliyasema hayo jana wakati akizungumza kwenye mkutano wa kampeni katika Jimbo la Mtama mkoani Lindi.
Alisema
Nape anaandaliwa njama ili asipite katika kinyang’anyiro cha ubunge
jimboni humo kwa sababu aliwataka baadhi ya wana-CCM wajivue gamba
wakati chama hicho kikiwa katika mchakato wa kufanya mabadiliko.
Hata
hivyo, Dk. Magufuli alisema Nape ni kiongozi mzuri ambaye endapo yeye
(Dk. Magufuli), angekuwa na uwezo wa kumhamisha, angemhamishia kwenda
kugombea katika jimbo lake la Chato.
Credit; Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment