ULE mjengo wa staa wa filamu Bongo, Elizabeth
Michael ‘Lulu’ ambao alimzawadia mama yake Lucresia Karugila, imedaiwa
umeshindikana kuuzika baada ya kutangaza kuupiga bei ya shilingi milioni
hamsini.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Lulu na mama yake walifikia uamuzi wa
kuupiga bei mjengo huo uliopo maeneo ya Kimara Saranga jijini Dar baada
ya kuona mazingira ya eneo hilo si mazuri hususan kipindi cha mvua
kutofikika kwa urahisi.
“Wamedhamiria kuipiga bei nyumba hiyo lakini wanashindwana na wateja
kutokana na pesa hiyo ndefu anayoitaka wakati kiuhalisia nyumba haina
hadhi.
“Isitoshe ile nyumba ndani inapasukapasuka sakafu huenda kwa sababu
ilianza kujengwa siku nyingi, hivyo wateja wengi wanakwamia shilingi
milioni 35 wengine milioni 40, pesa ambayo Lulu na mama’ke hawapo tayari
kuipokea,” alisema mpashaji huyo.
Kutokana na ishu hiyo paparazi wetu alimtafuta Lulu ambaye simu yake
iliita bila kupokelewa lakini mama Lulu alipotafutwa kuzungumzia ishu
hiyo alisema:
“Hii nyumba ni yetu hata kama tukiiuza kwani kuna tatizo gani sioni
kama kuna cha ajabu hapo mpaka mkae mnatufuatilia kiasi hicho,
nimeshasema hayo ni mambo yetu binafsi hayawahusu sababu hamkutusaidia
kujenga, nimetoka msibani bado nina majonzi sitaki kuongelea tena hayo
mamboº.”
Chanzo: GPL

Tuesday, 6 October 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment