Halmashauri
ya CCM Mkoa wa Geita imemvua ujumbe wa Mkutano Mkuu, Peter Mwininga
baada ya kudaiwa kukiuka maadili ya Umoja wa Vijana (UVCCM).
Licha
ya kukiuka maadili ya umoja huo, Mwininga anadaiwa kukisaliti chama
hicho wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliopita kwa kuwatukana
viongozi wa ngazi za juu kwa njia ya mtandao.
Akizungumza
baada ya kikao hicho juzi, Katibu wa Siasa na Uenezi CCM mkoani hapa,
Said Kalidushi alisema baada ya wajumbe wa halmashauri kuu kupokea
malalamiko na mapendekezo kutoka UVCCM, waliamua kumvua nafasi ya ujumbe
huo kutokana na kupungukiwa na sifa.
Kalidushi
alisema wakati wa kampeni Mwininga alikihujumu chama chao na kumfanyia
kampeni mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa, huku akijua wazi kuwa
ni kosa.
Katibu
wa UVCCM mkoani hapa, Mashaka Mshola alisema kitendo cha Mwininga
kuvuliwa nafasi aliyokuwa nayo kinatokana na usaliti na huo ni mwanzo wa
chama hicho kuwafukuza wasaliti.
Credit;Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment