Sunday, 4 October 2015

Tagged Under:

Riyama Awaasa Wasanii Wanaotumika Kutetea Matumbo ya Wanasiasa, Wakati…

By: Unknown On: 06:21
  • Share The Gag
  • Riyama Awaasa Wasanii Wanaotumika Kutetea Matumbo ya Wanasiasa, Wakati…

    Riyama Awaasa Wasanii Wanaotumika Kutetea Matumbo ya Wanasiasa, Wakati…
    Ungependa kujua kodi za kuingiza gari nchini?
    Tembelea : www.kodiyagari.com
    Habari wapendwa wangu Leo naomba kuongea na wewe MTANZANIA mwenzangu rafiki yangu unae Like na ku comment katika ukurasa wangu (kwenye mtandao wa Instagram) naamini wewe ndio balozi wangu utake nifikishia ujumbe wangu Kwa jamii inayo tuzunguka.
     Ndugu zangu kupiga kura ni haki ya kila MTANZANIA hivo shime tujitokeze kwa wingi kwa wale umri unao tu ruhusu kupiga kura angalizo usikubali kushurutishwa na mtu wa aina yeyote yule kwa kumchagua kiongozi anae mtaka yeye kwa maslahi yake, bali chagua kiongozi kwa matakwa yako na kwa maslahi ya watanzania walio wengi. Hatakama una mpenda msanii mfanya biashara mtu mwenye nyadhifa mbali mbali usikubali akushikie akili kwani tutambue kua kila aliae hushika kichwache usije kulia kwa kichwa cha mwenzako kura ni siri ya mtu binafsi hakikisha unaitunza katika kifua chako mpaka siku ya kupiga kura na unaitoa siri katika kalamu na karatasi .
    Hakikisha hufanyi makosa kwani ukifanya madudu hapatakua wa kumlaum siasa ni uhuru wa mtu kuchagua Chama akipendacho na mgombea amtakae sio kwa kushurutishwa au kwa danganya toto tusisahu kuna maisha baada ya uchaguzi.

    Ndugu zangu vipenzi vyangu wa fanya kazi wenzangu tunao wapigia debe waheshimiwa wetu na vyama vyetu tukumbuke wanatetea kazi zao kwa faida ya matumbo yao na familia zao, najua kuna tunaopenda siasa na pia kuna tunaofata mkumbo sasa basi tusi haribu kazi yetu na kutengeneza kazi za wenzetu.

    Tufanye siasa ila ile ya kunadi sera za chamachako na kumdani mgombea wako bila ya matusi bila kuchochea na kusababisha vurugu na mfarakano tuwaongoze wananchi tusiwapoteze kwani tupo kwa ajili ya kuelimisha tusijisahau tukawapotosha ikumbukwe kuwa hawa ndio mabosi zetu sisi katika kazi zetu na tusiupoteze uaminifu tulioujenga kwao toka hapo awali tuijenge tasnia yt na nchi yetu .
     Huko mlipo ndugu zangu naomba msisahau Vilio vyetu kilio kikubwa ni hati miliki picha hazita tusaidia hizo tunazo piga na waheshimiwa wetu balı haki miliki ndio msingi wa kazi zetu tunaibiwa sana tuna dhulumiwa sana misingi hii yote tukiangalia kwa umakini tunaijenga wenywe tupendane tushirikiane tuepuke bahasha za leo tukumbuke kuna kesho ambayo tutakua na watoto na wajukuu maslahi kwa wote Tanzania... Asante

    Chanzo GPL

    0 comments:

    Post a Comment