Sunday, 4 October 2015

Tagged Under:

Ndoa ya Wastara, Bond Baada ya Uchaguzi

By: Unknown On: 06:26
  • Share The Gag



  • SASA imethibitika kuwa ndoa kati ya muigizaji nyota wa filamu Wastara Juma na Mtangazaji BondSuleiman itafanyika mara baada ya uchaguzi mkuu ujao.
    Bond ambaye pia ni muigizaji, aliliambia gazeti hili kuwa wawili hao wameshafikia muafaka wa kuoana lakini Wastara yupo bize na kampeni, kwani baada ya kuanguka katika ubunge wa viti maalum kwa tiketi ya CCM, sasa anazunguka mikoani na Samia Suluhu ambaye ni mgombea mwenza wa John Magufuli jambo ambalo limesababisha washindwe kufanya maandalizi.
    “Unajua Wastara amejiingiza kwenye siasa na mimi nataka akomae kwani itakuja kutusaidia baadaye ndiyo maana tumekubaliana kuahirisha ndoa mpaka uchaguzi uishe ndipo tutapanga tena,” alisema.
    Chanzo: GPL

    0 comments:

    Post a Comment