Huku vuguvuga la uchaguzi likiendelea, leo mwigizaji maarufu
nchini Vicenti Kigosi aliyekuwa anaongoza mapambano ya mabadiliko ndani
ya UKAWA kabla ya kuhamia CCM ameandika ujumbe ufuatao kwa mashabiki
wake..
“..Kwanza kabisa ningependa kuwaambia wafuata mkumbo mpende kupanua akili zenu na si kupenda kupanua vidole 2.
Nashangazwa sana na wapinzani kusimama mbele ya adhara na kusema
kuwa tangia tumepata uhuru miaka 50 iliyopita serikali haijafanya
chochote na wewe unashangalia tena anayekwambia hivyo ni kiongozi
aliyekaa madarakani miaka 10 mwingine miaka miwili alafu sasa hivi hao
hao ndio wanakwambieni kuwa watawaletea mabadiliko s'tukeni watanzania
watatuingiza mkenge hawa wapinzani.
Ninaamini watanzania wanataka kupata m badala wa ccm kwa kipindi
kirefu lkn mm naona bado kuwepo mbadala wa ccm maana hao ndio walewale
waliotoka ccm. pateni uzoefu kwanza kwa sasa bado mtatupeleka gizani.
Baadhi ya watu wanasema kuwa wasanii wanaowasapoti ccm
hawatonunua kazi zao wanamuziki wakiomba wapigiwe kura eti waambieni ccm
wawapigie kura wanasahau kwamba msanii naye ana haki ya kuwa upande wa
chama anayeutaka yeye kuna mifano mingi marekani wasanii walimsapoti
obama nigeria wasanii walimsapoti muhammadu buhari.sio sisi wakwanza
kufanya hivyo…” Ray kigosi
Chanzo GPl
Sunday, 4 October 2015
Tagged Under:
Nini maoni yako juu ya kauli hii ya Ray kuhusu yeye kuikimbia Team Mabadiliko?
By:
Unknown
On: 06:14
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment