SIKU Chache baada ya muigizaji wa siku nyingi,
Mahsein Awadhi Said ‘Dk. Cheni’ kutoa tamko juu ya kumuoa ‘mtoto mkubwa’
katika tasnia hiyo, Elizaberth Michael Kimemeta ‘Lulu’, binti huyo
mwenye mvuto amesema hakuna mtu wa kumzuia kuwa karibu na Dk. Cheni huku
akishikilia alichokisema…. “mambo yetu hayamhusu mtu”, Amani
linaandika.
Muda mfupi baada ya Dk. Cheni kusema haoni tatizo kwa kumuoa Lulu,
gazeti hili lilimtafuta msanii huyo kwa njia ya simu “Mtu anayesimama
na wewe wakati wa shida ndiye rafiki kwa kweli, Dk. Cheni amenisaidia
pale ambapo kila mtu alijitenga nami, kama kuna kinachoendelea kati
yetu, ni cha kwetu na mambo yetu,” alisema.
Chanzo: GPL
Sunday, 4 October 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment