Msanii wa maigizo, muimbaji, Mtunzi, Mpanga Muziki na Mchekeshaji
Patcho Mwamba ameendelea kuongeza fani ambazo amekuwa akizimudu vyema
kwa upande wa sanaa, huku akiwa katika maandalizi ya kutoa albam mpya ya
bendi ya FM Academia.
Star huyo amejipanga kwa ajili ya kutengeneza kipindi kitakachosimama
kwa jina la Bana Congo ambacho atawafahamisha mashabiki zaidi juu yake
mara baada ya uchaguzi.
Patcho ameiambia eNewz kuwa kwa sasa hana filamu yoyote kubwa ambayo
anatayarisha kama yeye, isipokuwa amekuwa akishiriki katika filamu za
watu hapa na pale, kuonesha kuwa hajaweka uigizaji pembeni, akiendelea
kujijengea sifa kubwa ya kuwa kati ya wasanii wachache wenye uwezo wa
kufanya mambo mbalimbali kwa kiwango cha juu kwa wakati mmoja.
EATV.TV
Chanzo GPL.
Sunday, 4 October 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment