MKALI wa filamu hapa nchini, Gabo Zigamba, amedai kwamba anaweza kusambaza kazi zake mwenyewe bila ya kuwategemea Wahindi.
Msanii huyo amedai kwamba filamu yake ya ‘Safari ya Gwalu’ alifanikiwa
kuisambaza mwenyewe kupitia kampuni yake ya D Entertainment, hivyo hana
ulazima wa kutegemea watu binafsi.
“Nilikuwa kama najaribu kuisambaza kazi hiyo mimi mwenyewe,
nimegundua kwamba inawezekana kwa kuwa nimeweza kusambaza Tanzania mzima
kupitia kampuni yang“u. Hivyo sioni sababu ya kuwategemea Wahindi
kuweza kusambaza kazi zangu, nimeuza kazi nyingi sana na bado watu wanaendelea kuzihitaji.
Chanzo; Mtanzania
Thursday, 14 January 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment