Tuesday, 26 January 2016

Tagged Under:

JK akabidhi ripoti ya jopo lake UN

By: Unknown On: 23:51
  • Share The Gag

  • Rais Mstaafu, Dk Jakaya Kikwete.

    MWENYEKITI wa Jopo la Ngazi ya juu kuhusu Mwitikio wa Kimataifa wa Majanga ya Kiafya, Rais mstaafu Jakaya Kikwete juzi amemkabidhi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ripoti ya jopo lake. Aprili mwaka jana, Ban Ki moon alimteua Kikwete kuongoza jopo lililokuwa na wajumbe watano.
    Kwa mujibu wa hadidu za rejea jopo hili lilitakiwa kutekeleza majukumu yake kuanzia mwezi Mei hadi Desemba 2015. Akipokea ripoti hiyo katika hafla fupi mjini New York, Ban Kimoon, pamoja na kushukuru jopo hilo amesisitiza kwamba, ushauri na mapendezo yaliyotolewa na jopo hilo yatazingatiwa na kufanyiwa kazi.
    Alisema pia itasaidia katika kutoa mwongozo kwa Jumuiya ya Kimataifa juu ya namna ya kuimarisha na kuboresha miundombinu ya afya ili iweze kukabiliana na magonjwa ya milipuko. Ban Ki-moon amelihakikishia Jopo hilo kuwa Ripoti hiyo itawekwa hadharani mapema ili nchi wanachama wa UN na makundi mbalimbali ya jamii waweze kuisoma.
    Naye Mwenyekiti wa Jopo, Kikwete amemshukuru Ban Kimoon, kwa kumpatia heshima ya kuongoza jopo hilo linaloundwa pia na Celso Amorim (Brazil), Micheline Calmy (Uswisi), Marty Natalegawa (Indonesia), Joy Phumapi (Botswana) na Rajav Shah (Marekani).
    Jukumu kubwa la jopo hilo ilikuwa ni kutoa mapendekezo ya namna ya kuimarisha mifumo ya kitaifa na kimataifa katika kuzuia na kukabiliana na majanga ya kiafya yakiwamo magonjwa ya mlipuko, ikiwa ni pamoja na kujifunza kuhusu mwitikio wa Jumuiya ya Kimataifa kufuatia kuibuka kwa janga la ugonjwa wa ebola.
     Chanzo Gazeti la HabariLeo.

    0 comments:

    Post a Comment