Nuh Mziwanda amedai kuwa aliyofanyiwa na Shilole ni mengi na mazito
ambayo ilibidi ayafiche kwa maslahi ya penzi lao na heshima kwake.
Akiongea kwenye kipindi cha D’Weekend Chat Show cha Clouds TV Ijumaa
hii mbele ya Shilole aliyekuwa amejikunyata pembeni kwa kukasirishwa na
uwepo wa ex wake studioni hapo bila kutaarifiwa mwanzoni, Nuh alisema
Shilole hakuwa mwanamke wa kutawaliwa.
“Yeye anajua mambo gani alikuwa anafanya kwangu mambo ambayo yalikuwa
hayastahili anifanyie. Alikuwa anafanya kwa kunichukulia poa kwamba
nitafanya nini lakini at end of the day kila kitu kina mwanzo na
mwisho,” alisema.
Nuh alisema ni ngumu tena kurudisha imani kwa mpenzi wako huyo licha
ya kukiri kuwa bado hajaweza kuwa tayari kuwa na mwanamke mwingine kwa
sasa.
Chanzo: Bongo5
Sunday, 17 January 2016
Tagged Under:
Nuh Mziwanda: Nilishaficha Mambo Mengi Sana Mabaya ya Shilole kwa Maslahi ya Penzi Letu
By:
Unknown
On: 23:29
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment