Friday, 22 January 2016

Tagged Under:

Kardinali Pengo Aruhusiwa Kutoka Muhimbili

By: Unknown On: 00:58
  • Share The Gag

  • Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo aliyekuwa amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Muhimbili ameruhusiwa baada ya afya yake kuimarika.

    Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Profesa Mohammed Janabi alisema jana kuwa Kardinali Pengo aliruhusiwa saa 6.30.

    Awali, Profesa Janabi alisema Kardinali Pengo alilazwa katika kitengo hicho mwaka jana kabla ya kuruhusiwa siku 10 baadaye baada ya kupata nafuu na alipewa siku tisa kurudi hospitalini hapo kwa ajili ya kuendelea kufuatilia zaidi afya yake.

    Kardinali Pengo alilazwa katika kitengo hicho Desemba 31 mwaka jana na kuruhusiwa siku 10 baadaye. Januari 18 alirudi hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu ya ufuatilizi kabla ya jana kuruhusiwa.    
    Credit;Mpekuzi blog

    0 comments:

    Post a Comment