MISS Tanzania 2006, ambaye pia ni mwigizaji wa filamu za bongo, Wema
Sepetu, amewataka wabunifu chipukizi wa mavazi na mitindo nchini
walitumie vizuri jukwaa la mitindo la Lady In Red Fashion Show 2016, ili
wafikie malengo waliyojiwekea.
Wema alitoa rai hiyo alipokuwa akizungumza nao kuhusiana na onyesho
litakalofanyika Januari 31, katika ukumbi wa Danken House, uliopo
Mikocheni, jijini Dar es Salaam.
“Kwa sasa mnatakiwa muwe wabunifu zaidi mje na vitu vya kipekee ili
kazi hizo ziwe chachu na kivutio kwa wateja wenu, pia iwaongezee
mashabiki wa mavazi na ajira yenu, iwe ya uhakika na soko,’’ alieleza
Wema.
Naye Mkurugenzi wa Fabak Fashions na muandaaji wa jukwaa hilo, Asia
Idarous, alisema jukwaa hilo ni shule na daraja la wabunifu wa mavazi na
mitindo, hivyo litaendelea kuenziwa ili lizidi kuzalisha wabunifu wengi
zaidi.
Chanzo; Mtanzania
Wednesday, 20 January 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment