Sunday, 31 January 2016

Tagged Under:

Apendekeza wakimbizi wapigwe risasi Ujerumani

By: Unknown On: 06:15
  • Share The Gag
  • Apendekeza wakimbizi wapigwe risasi Ujerumani
    Mwanasiasa mmoja mbishi nchini Ujerumani ameibua hasira kubwa, baada ya kupendekeza kuwa maafisa wa polisi wanafaa kuruhusiwa kuwapiga risasi wahamiaji, wanaojaribu kuingia nchini humo bila idhini.
    Kiongozi mkuu wa chama cha mrengo wa kulia cha Alternative for Germany Frauke Petry, ameliambia gazeti la Mannheimer Morgen, kwamba anapendekeza matumizi ya silaha kwa polisi kama hatua ya mwisho.
    Frauke Petry, wa chama cha Alternative for Germany ameliambia gazeti la Mannheimer Morgen, anapendekeza matumizi ya silaha Sheria za polisi wa Ujerumani zinasema kuwa hakuna sheria inayodhinisha kushambulia wakimbizi kwa risasi.
    Mwanachama mmoja mkuu wa chama cha Social Democrats, amemkumbusha Frauke Petry kwamba, mwanasiasa wa mwisho wa iliyokuwa Ujerumani mashariki, ambaye alimuru wakimbizi kupigwa risasi, alikuwa Erich Honecker, kiongozi mkuu wa utawala wa kikomunisti ambao ulisambaratika mwaka 1989.

    Chanzo BBC Swahili.

    0 comments:

    Post a Comment