NA MWALI IBRAHIM
MKALI wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Nasib Abdul ‘Diamond’
ameshangazwa na watu anaodai ni wakubwa kwake kutaka kushindana naye
wakati yeye ni zaidi yao.
Diamond alisema anashangazwa na wanaohangaika kushindana naye wakati
yeye anajulikana zaidi yao, akaunti yake haikosi milioni 10 na pia ana
mashabiki wengi kwenye mitandao ya kijamii.
“Mi nashangaa wasanii wengi wananizonga kuhusu mtoto wangu wanataka
nikapime DNA, wao inawahusu nini kama wa kwangu ama si damu yangu, mimi
nawashangaa watu wazima wanataka kushindana na mtoto mdogo ambaye kwanza
ni staa zaidi yao, najulikana kila nchi niendayo, akaunti yangu haikosi
milioni 10, Instagram nina mashabiki wengi kuliko wao, mimi naona bora
wapambane kutangaza muziki wao na kujenga nyumba nzuri za kuishi,’’
alijinadi Diamond kupitia kipindi cha Amplify kinachoongozwa na
mtangazaji Milard Ayo.
Hayo yalikuwa majibu ya msanii huyo baada ya kuibuka kwa uzushi
katika mitandao ya kijamii na mijadala mbalimbali kwamba wasanii wengi
wamekuwa wakidai kuwa Tifah si mtoto wake na wanamtaka akapime vinasaba
‘DNA’, kitu ambacho kinamkera ndiyo maana akawataka wamuache na maisha
yake nao wahangaikie muziki wao.
Chanzo Mtanzania.
Friday, 22 January 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment