Korea Kaskazini imesema imemkamata mwanafunzi kutoka Marekani ambaye anadaiwa kufanya “kitendo cha uchokozi” dhidi ya taifa.
Shirika
la habari la serikali KCNA limesema serikali ya Marekani ilikuwa
“imemvumilia na kumtawala kwa werevy” mwanafunzi huyo, ambaye husomea
Chuo Kikuu cha Virginia.Mwanafunzi huyo ambaye jina lake halijatolewa anadaiwa kuingia Korea Kaskazini kama mtalii, na inadaiwa “alilenga kuvunja umoja wa taifa hilo”.
KCNA haijatoa maelezo zaidi, lakini mwanafunzi huyo anaendelea kuchunguzwa.
Afisa wa ubalozi wa Marekani katika taifa jirani la Korea Kusini ameambia shirika la habari la Reuters kwamba hawana habari kuhusu kukamatwa kwa mwanafunzi huyo.
Ikithibitishwa, basi mwanafunzi huyo atakuwa wa tatu kutoka nchi za Magharibi kuzuiliwa nchini Korea Kaskazini.
Mhubiri kutoka Canada na mwanamume mwingine Mkorea-Mmarekani pia wanazuiliwa na maafisa wa taifa hilo.
Chanzo BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment