MKALI wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’ (Diamond
Platinum), amesema pindi atakapoacha muziki atatumikia siasa huku
akitamani kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Msanii huyo aliweka wazi mpango wake huo hivi karibuni alipohojiwa
katika kipindi cha Papaso kinachoongozwa na mtangazaji, Di’jaro Arungu
ambapo aliweka wazi kwamba akiingia katika siasa atalenga kuwa Waziri wa
Michezo pindi Waziri Nape Nnauye atakapomaliza muda wake.
“Kwa hivi sasa bado sijaingia kwenye siasa ila nikiingia baadaye
atakapomaliza Nape nafasi yake nitachukua mimi,’’ alieleza na kuongeza:
“Kile cheo nakiweza kwa sababu mambo ya mpira, movie nayaweza na
nikiwa waziri nitavifanya viweze kuleta maendeleo makubwa,” alieleza
bila kufafanua atabadilishaje viwe vya maendeleo tofauti na wanavyofanya
viongozi wa sasa.
Hata hivyo, Diamond hakuweka wazi kwamba ataingia kwenye siasa kupitia chama gani na mwaka gani.
Chanzo Mtanzania
Thursday, 28 January 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment