William Mtitu akiwa na JB
KAIMU Mwenyekiti wa Chama cha Maprodyuza Tanzania, William Mtitu,
amesema hakuna prodyuza atakayeruhusiwa kufanya kazi ya kutengeneza
filamu ndani na nje ya nchi kama hatasajiliwa na chama hicho.
Mtitu alisema chama hicho kimeamua hayo ili kuondoa filamu zisizo na
ubora katika soko la filamu nchini ambalo anadai limejaa filamu zisizo
na ubora hali inayopelekea kudharauliwa na mashabiki wa kazi hizo.
“Wakati wa kufanya filamu kwa mazoea umepita, kwanza lazima prodyuza
awe na elimu ya kazi hiyo kisha asajiliwe bila kufanya hivyo hatopata
leseni ya utambuzi wa kuwa mwanachama mwenye sifa za kufanya kazi hizo
za uprodyuza wa filamu,” alisema Mtitu.
Mtitu aliongeza kwamba kazi hiyo itaendeshwa bila kuangalia umaarufu
wa mtu ama ukongwe wake kwenye kazi hiyo hivyo ni usajili kwa mwaka huu
ni lazima ili tuboreshe kazi za filamu na soko lake linaloelekea
kuporomoka.
Mtanzania
Saturday, 16 January 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment