Mkali wa filamu Bongo, Rammy Gallis ‘Pacha wa Kanumba ’ anadaiwa kuishi
nchini bila vibali maalum, jambo linalomuweka hatarini muda wowote
kuweza kutimuliwa Bongo kutokana na tumbuatumbua ya Serikali ya Rais
John Pombe Magufuli inayoendelea.
Kwa mujibu wa chanzo, kuna hatihati kubwa ya msanii huyo ambaye wengi
wamezoea kumuita Msomalia kufungashiwa virago kwani hana uhalali wa
kuendelea kuwepo nchini.
“Yaani kwa hii kasi ya Mh. Magufuli sidhani kama Rammy atasalimika,
si unaona jinsi ambavyo mzee wa kutumbua majipu yupo makini kwenye
uongozi wake, yule kaka ni mkimbizi yaani akae tayari kwa safari ya
kurudi kwao huko,” kilisema chanzo.
Baada ya kupata madai hayo, Showbiz Xtra ilimpo-vutia waya msanii huyo ili kusikia kauli yake kufuatia madai hayo alijibu;
“Mimi ni Mtanzania halali nina vigezo vya kuwepo Bongo, mama yangu ni Msomali baba ni Muarabu kachanganya na Mbrazil.”
Chanzo: GPL
Thursday, 28 January 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment