Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imefuta kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi
wa Ubunge, iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa kiti hicho kupitia
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba, dhidi ya Mbunge wa Kawe,
Halima Mdee.
Jaji
Zainabu Mruke alitoa uamuzi huo jana, kwa kuwa Warioba aliomba kuondoa
shauri hilo mahakamani baada ya kukubali hoja za pingamizi la awali
zilizowasilishwa na Mdee pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).
Warioba
alifungua kesi ya uchaguzi akipinga matokeo yaliyompa udhindi Mdee,
dhidi Mwasheria Mkuu wa Serikali na Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo,
ambaye ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni pamoja na Mdee.
Katika
kesi hiyo namba 7 ya mwaka 2015, Warioba alikuwa akiiomba mahakama hiyo
ibatilishe matokeo ya uchaguzi huo pamoja na mambo mengine, kwa kuwa
haukuwa huru na wa haki.
Hata
hivyo, Mdee pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali waliwasilisha,
pingamizi la awali, wakiomba mahakama itupilie mbali kesi hiyo, lakini
wakati wa kusikiliza pingamizi, Warioba kupitia, wakili wake Emmanuel
Makene alikubaliana na hoja za pingamizi hilo na kuomba mahakama iondoe
kesi hiyo.
Akitoa
uamuzi jana, Jaji Mruke alisema, kwa kuwa mdai amekubali hoja za
pingamizi na ameamua kuiondoa mahakamani kesi hiyo, basi mahakama
inaamuru kesi iondolewa.
Credit; Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment