Saturday, 16 January 2016

Tagged Under:

Watu 21 wauawa katika shambulizi Burkina faso

By: Unknown On: 22:22
  • Share The Gag
  • Burkina faso
    Rais wa Burkina Faso amesema takriban watu 21 wameuwawa katika shambulio kwenye hoteli moja mjini Ogadugu na wanamgambo waliovamia hotel hiyo.
    Roch Mark Christian Kabore amesema washambuliaji wanne waliovamia hotel hiyo waliuliwa ambapo wawili kati yao ni wanawake. Shambulio hilo lililotokea kwenye hotel ya Splendide kwenye mji mkuu wa Ouagadougou sasa limemalizwa.
    baadhi ya manusura Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo amesema wanamgambo hao wameuwa watu kumi na nane kutoka mataifa mbalimbali. Zaidi ya watu mia moja na ishirini walikimbia hotel hiyo maarufu kwa watalii.
    walionusurika wanasema wanamgambo hao walianza kupiga risasi kwenye jengo hilo na kisha kuliwasha moto.
    Eneo lililo karibu na jhoteli ya Splendid ilioshambuliwa Wapiganaji wanne waliuawa aliongezea huku watu 21 wa mataifa 18 tofauti wakifariki wakati wa shambulio ambalo pia liliulenga mgahawa huo.
    Vikosi maalum vya Ufaransa vinasaidia wanajeshi wa taifa hilo katika oparesheni hiyo.
    Eneo lililoshambuliwa Rais wa Ufaransa Francois Hollande ameshtumu shambulio hilo la taifa hilo ambalo lilikuwa koloni yake hapo zamani.
    Kundi la Al-Qaeda la islamic Maghreb{AQIM} limesema kuwa lilitekeleza shambulio hilo katika taifa hilo la Magharibi mwa Afrika.
    Hoteli ya Splendid Mnamo mwezi Novemba shambulio la AQIM katika hoteli moja ya Bamako nchini Mali liliwauwa watu 19.
    Chanzo BBC Swahili.

    0 comments:

    Post a Comment