Wednesday, 20 January 2016

Tagged Under:

20 wauawa kwenye shambulizi Pakistan

By: Unknown On: 04:13
  • Share The Gag
  • Taliban wanasema kuwa shambulizi hilo ni la kulipiza kisasi oparesheni ya kijeshi dhidi ya ngome zake
    Shambulizi linalokisiwa kuendeshwa na wanamgambo wa Taliban katika chuo kimoja kaskazini magharibi mwa Pakistan limesababisha vifo vya karibu watu 20 na kuwajeruhi wengine 50.
    Karibu saa tatu tangu kuanza kwa shambulizi hilo afisa mmoja wa kijeshi alisema kuwa ufytuaji wa risasi umekwisha lakini wanajeshi walikuwa wakiendesha msako katika chuo cha Bacha Khan kilicho eno la Charsadda.
    Jeshi lilisema kuwa washambuliaji wanne waliuawa huku Taliban wakisema kwa washambuliaji wanne wa kujitoa mhaga walihusika kwenye shambulizi hilo.
    Taliban waliwaua wanafunzi 130 kwenye shule moja katika mji ulio karibu wa Peshawar mwaka 2014.
    Msemaji wa Taliban aliliambia shirika la habari la AFP kuwa shambulizi hilo ni la kulipiza kisasi oparesheni ya kijeshi dhidi ya ngome za Taliban.
    Siku chache zilizopita baadhi ya shule katika mji wa Peshawar zilifungwa kufuatia ripoti kuwa wanamgambo walikuwa wakipanga mashambulizi.

    Chanzo BBC Swahili.

    0 comments:

    Post a Comment