Manejimenti ya sahara media group ambao ni wamiliki wa Star Tv, RFA na Kiss Fm imesema haijapata barua au taarifa rasmi yeyote kutoka mamlaka ya mawasilano Tanzania TCRA ya kutakiwa kufunga vyombo vyake.
Imesema
wameshtushwa na taarifa hiyo ikizingatiwa kwamba wamekuwa wakilipia
leseni ada zake na ada za masafa kwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni
500 hadi kufikia mwezi October 2015.
Wamesema
yamekuwapo mawasiliano ya mara kwa mara kati ya TCRA kanda ya Mwanza,
makao makuu na sahara media group limited nakukubaliana juu ya utaratibu
wa malipo ya ada husika.
Lakini
menejimenti imeshangazwa na hatua hiyo ya TCRA kutangaza kuvifungia
vituo vyake kupitia mkutano wa vyombo vya habari bila kujali athari
zakufungia vyombo vya kitaifa kwa walaji na watoa huduma.
Sahara
media group limited imekuwa ikilalamikia utozwaji wa ada kwa dola za
kimarekani jambo ambalo limekuwa likipandisha ada hizo kila mara na
kufanya ulipwaji wa ada hizo kibajeti kukwama kwama.
Menejimenti
pia imelaani taarifa hiyo kutolewa mwishoni wa wiki nakuvipa vituo
husika siku mbili tu kukamilisha ulipaji ada wakijua dhahiri jumamosi na
jumapili sio siku za kazi.
Menejimenti
ya star tv inawaondoa wasiwasi watazamaji na wasikilizaji wake,
hatua thabiti zitachukuliwa ili kumaliza tatizo hili kwa sahara media
group limited na TCRA Kwa Kufuata Misingi Ya Sheria, Kanuni Na
Maridhiano.
Credit; Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment