Nigeria inaomba
mkopo wa dharura wa jumla ya dola bilioni tatu unusu kutoka kwa Benki ya
Dunia kujaribu kuziba pengo kwenye bajeti yake.
Uchumi wa Nigeria umeathiriwa sana na kushuka kwa bei ya mafuta duniani.Waziri wa fedha nchini humo Kemi Adeosun amesema amekuwa akifanya mazungumzo na maafisa wa Benki ya Dunia.
Hatua ya Nigeria kuomba mkopo wa dharura inashangaza ikizingatiwa kwamba siku chache zilizopita Shirika la Fedha Duniani (IMF) lilisema haihitaji usaidizi wa kifedha.
Serikali mpya ya Rais Muhammadu Buhari ilikuwa imeacha pengo katika ufadhili wa bajeti yake katika juhudi za kujaribu kusisimua uchumi wa taifa.
Lakini tofauti kati ya mapato na matumizi imeendelea kuongezeka na kuilazimu Nigeria kuomba usaidizi kutoka nje.
Nigeria silo taifa la pekee kuathiriwa na kushuka kwa bei ya mafuta duniani.
Azerbaijan, nchi nyingine inayozalisha mafuta kwa wingi, pia imeanza mazungumzo na Benki ya Dunia.
Uchumi wa Venezuela nao umekuwa katika hali ya tahadhari.
Kushuka kwa bei ya mafuta kulichangia sana katika kushuka kwa jumla ya mapato ya taifa Urusi mwaka jana.
Chanzo BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment