Wednesday, 13 January 2016

Tagged Under:

Marekani ‘yaiomba radhi’ Iran kuhusu boti

By: Unknown On: 01:12
  • Share The Gag
  • Boti ya Marekani aina ya Riverline, ambayo ni sawa na mbili zilizokamatwa na Iran
    Marekani imeomba radhi kutoka kwa Iran baada ya mabaharia 10 wa Marekani kuingia maeneo ya bahari ya Iran, kamanda wa kikosi cha jeshi la Iran amesema.
    Jenerali Ali Fadavi, anayeongoza kitengo cha wanamaji cha jeshi la Revolutionary Guards, amesema mabaharia hao wanaozuilia walitenda vitendo “visivyo vya kitaalamu”.
    Lakini amedokeza kwamba wanamaji hao, wanaozuiliwa na wanajeshi wa Revolutionary Guards, wataachiliwa huru hivi karibuni.
    Wanajeshi wa Revolutionary Guards hulinda serikali ya Kiislamu ya Iran pamoja na kuzuia uingiliaji kutoka kwa mataifa ya kigeni na kuzuia mapinduzi ya kijeshi na maasi.
    Taifa hilo huwa pia na wanajeshi wa kawaida ambao hulinda mipaka na kudumisha Amani na utulivu ndani ya nchi. accused those Licha ya mafanikio makubwa mwaka jana kuhusu mkataba wa nyuklia, uhasama bado umeendelea baina ya Marekani na Iran.
    Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani John Kerry amewasiliana na mwenzake wa Iran Javad Zarif kuhusu kisa hicho.
    Akitoa tathmini yake kuhusu mazungumzo hayo, Jenerali Fadavi amesema "Bw Zarif alikuwa na msimamo mkali, akisema mabaharia hao waiingia maeneo yetu baharini na hawakufaa, na akasema Marekani wanafaa kuomba radhi”.
    "Hili limefanyika na haitachukua muda mrefu, na jeshi la wanamaji, kwa mujibu wa uongozini jeshini, litachuku hatua mara moja likipokea maagizo,” ameongeza.
    Marekani awali ilikuwa imesema wanamaji hao walikuwa kwenye mazoezi kati ya Kuwait na Bahrain boti zao mbili zilipopata hitilafu za kimitambo na wakaingia maeneo ya bahari ya Iran.

    Chanzo BBC Swahili.

    0 comments:

    Post a Comment